Serikali ya Kenya imepiga marufuku uchinjwaji wa punda, je ni kwanini?

Punda nchini kenya wanakabiliwa na uwezekano wa kutoweka mwaka 2030 ikiwa hawatalindwa
Maelezo ya picha, Punda nchini kenya wanakabiliwa na uwezekano wa kutoweka mwaka 2030 ikiwa hawatalindwa

Serikali ya Kenya imetangaza marufuku ya uchinjwaji wa punda nchini humo ili kuzuia kutokomea kwa wanyama hao ambao idadi yao inasemekana kupundua.

Waziri wa kilimo Peter Munya alitangaza kufungwa kwa kufungwa kwa vichinjio vyote vya punda baada ya wakulima kuandamana nje ya ofisi yake wakidai kutoweka kwa punda ambao huwasaidia kubeba mizigo kutawaathiri.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika linalotetea maisha ya wanyama -Africa network for Animal Welfare punda nchini kenya wanakabiliwa na uwezekano wa kutoweka mwaka 2030 ikiwa hawatalindwa.

''Sasa hivi bei ya punda imefikia kati ya shilingi 15,000 , elfu 20,000 kwasababu punda wamechinjwa, wameliwa na wachina'', alisema mmoja wa wakulima wenye hasira katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Kenya''.

Waziri Peter Munya alisema: ''Tunawapatia kipindi cha mwezi mmoja wamiliki wa vichinjio vya punda kubadili vichinjio hivyo kuvibadili kuwa vichinjio vya wanyama wengine wa kawaida.

Uchina ni mnunuzi mkuu wa nyama na bidhaa za punda nchini Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchina ni mnunuzi mkuu wa nyama na bidhaa za punda nchini Kenya

Tangazo la marufuku ya vichinjio vya punda limekua ni ahueni kwa wakulima na wanaharakati wa haki za wanyama ambao kwa muda wamekua wakipinga kuchinjwa kwa nyama ya punda nchini Kenya.

Kwa miaka kadhaa wamekua wakiandamana katika ameneo ya Baringo, Machakosi na Turkana wakidai kuongezeka kwa uhitaji wa nyama ya punda kumesababisha kuongezeka kwa wizi wa punda.

Idadi ya Punda nchini Kenya imekuwa ikipungua.

Kundi hilo la mtandao wa watetezi wa haki za wanyama, (ANAW) lilimesema kuwa punda wamekuwa wakitoweka haraka sana.

Ripoti ilisema tangu kufunguliwa kwa maeneo manne ya machinjio ya punda kwa ajili ya biashara mwaka 2016, ''idadi kubwa ya wanyama hao huchinjwa kila siku''.

Inakadiriwa kuwa punda 410 huuawa kila siku.

Ripoti imeongeza kuwa suala hilo lilishawekwa wazi mwaka 2017. Wakati huo BBC iliporipoti kuhusu madai ya watu kulalamika kuibwa kwa punda wao ili kupelekwa kwenye soko.

Lakini mkuu wa machinjio amesema: ''tunafurahia wachina, kwasababu awali tulikuwa hatupati chochote kutokana na punda, lakini watu wengi sasa.

Inakadiriwa kuwa punda 410 huuawa kila siku nchini Kenya, kwa mujibu wa shirika la haki za wanyama (ANAW)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Inakadiriwa kuwa punda 410 huuawa kila siku nchini Kenya, kwa mujibu wa shirika la haki za wanyama (ANAW)

Shirika moja linalohusika na maslahi ya wanyama nchini Kenya, linasema bei ya Punda imepanda mara dufu nchini humo kwa sababu ya nyama ya mnyama huyo kuongezeka hasa katika taifa la china taifa ambalo hununua kwa wingi bidhaa ya mnyama huyo

Kwa mujibu wa shirika hilo, sababu ya bei ya Punda kupanda kwa karibu asilimia 200 ni kutokana na ongezeka la biashara ya bidhaa za mnyama huyo huko Uchina ambako nyama ya punda ni kitoweo kilicho na walaji wengi.

Si mara ya kwanza kwa watetezi wa haki za wanyamapori kudai vichinjio vya punda vifungwe

Kundi jingine la mtandao wa watetezi wa haki za wanyama, (ANAW) lililisema kuwa punda wamekuwa wakitoweka haraka sana.

Ripoti yake ilisema tangu kufunguliwa kwa maeneo manne ya machinjio ya punda kwa ajili ya biashara mwaka 2016, ''idadi kubwa ya wanyama hao huchinjwa kila siku''.

Inakadiriwa kuwa punda 410 huuawa kila siku.

Ripoti pia iliongeza kuwa suala hilo lilishawekwa wazi mwaka 2017. Wakati huo BBC iliporipoti kuhusu madai ya watu kulalamika kuibwa kwa punda wao ili kupelekwa kwenye soko.

Lakini mkuu wa machinjio amesema: ''tunafurahia wachina, kwasababu awali tulikuwa hatupati chochote kutokana na punda, lakini watu wengi sasa

Punda ni mnyama wa kubeba mizigo na kufanya kazi ya sulubu, lakini nyama yake sasa imekuwa kitoweo
Maelezo ya picha, Punda ni mnyama wa kubeba mizigo na kufanya kazi ya sulubu, lakini nyama yake sasa imekuwa kitoweo

Mataifa kadhaa ya kiafrika yamepiga marufuku uuzaji ya nyama na bidhaa nyenginezo za punda, kwa ajili ya soko hilo la Uchina, kwa sababu punda ambao hutumiwa zaidi kwa ajili ya kusaidia kubeba mizigo mashambani, sasa idadi yao inapungua kwa kasi mno.

Kuna hofu kuwa huenda baadhi ya watu wanawasafirisha punda kimagendo hadi machinjioni kutokana na kupanda kwa bei yake.

wananufaika.''

Shirika la kuteteta haki za wanyama lilitaka machinjio yote ya wanyama hao yafungwe.

Ripoti ya shirika hilo inakadiria uwepo wa punda 900,000 mpaka milioni 1.8 nchini Kenya.

Maelezo ya sauti, Hospitali ya kipekee inayowahudumia punda Kenya

Mataifa mengi yamepiga marufuku uchinjaji wa punda yakiwemo mataifa kadhaa ya Afrika kama vile Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso, Mali, na Senegal.

Mataifa hayo aidha yameipiga marufuku China kununua ngozi ya punda kwani huenda ikamaliza kabisa wanyama hao duniani.

Soko kubwa la ngozi ya punda pia imeongezeka nchini Afrika Kusini.